• Latest News

    Sunday, 31 July 2016

    FANGASI KATIKA VIDOLE VYA MIGUU|ATHELETES FOOT

    Athlete's foot ni aina ya ugonjwa wa ngozi unaotokea katikati ya vidole vya miguu (in between toes)..Huwasha,na mara nyingi hufunikwa na gamba nyeupe kati ya vidole vya miguu..Na mara nyingi huwa kati ya kidole cha nne na cha tano cha mguu!
    Hii hali sio mara zote ni fangasi pekee hata bakteria huweza kuleta hali hiyo au mchanganyiko wa wadudu hao wote kwa pamoja.

    Hali hii hujitokeza sana kwa watu wanaovaa viatu vya raba au boots na plastic sandshoes..Hali hii isipotibiwa mapema huleta harufu na tiba yake kuwa ngumu au complicated.

    KINGA NA TIBA

    -Weka ukavu katikakati ya vidole vyako vya miguu..Hii unaweza kulifanya pale unapooga au kunawa hakikisha unajikausha vyema sehemu hizo (keep the space in between the toes dry)
    -Tumia betadine scrub au GV
    -Tumia soksi za pamba na usivae viatu vinavyobana na kuleta joto miguuni
    -Kubadili soksi kila siku kunasaidia kuzuia kupata maambukizi tena

    -Tumia Imidazole cream au whitefield ointment kila siku mara mbili kwa muda wa wiki au zaidi na mara nyingi mpaka wiki 4.

    Karibu buswelu pharmacy, Ilemela Mwanza kwa ushauri na tiba +255767650213.

    Saturday, 30 July 2016

    Mkurugenzi Mtendaji wa Bagamoyo atumbuliwa

    Rais magufuli ameendelea kutumbua watendaji serikalini kwa kutoridhishwa na utendaji..Taarifa ya Ofisi ya Tamisemi iliyotolewa jana imesema mkurugenzi wa Bagamoyo ametenguliwa siku chache tu baada ya uteuzi kutokana na utendaji usiordhisha!Unaonaje hatua hiyo?

    Friday, 29 July 2016

    Majengo Ya Serikali Dar Kupigwa Mnada Baada Ya Kuhamia Dodoma

    RAIS MAGUFULI KUPIGA MNADA MAJENGO YA SERIKALI
    Rais JOHN MAGUFULI amesema kuwa baada ya kukamilika kwa taratibu za kuhamishia makao makuu ya Serikali mjini Dodoma, atapiga mnada majengo yote ya Serikali ili kupata Fedha za Ujenzi wa mji mkuu huo.
    Rais MAGUFULI amesema hayo wakati akihutubia mkutano wa hadhara mjini Manyoni mkoani SINGIDAakisisitiza juu ya azma yake ya kuhamishia Makao makuu DODOMA.
    Source:TBC Habari

    Buswelu Pharmacy-Ilemela,Mwanza

    Outside look of our pharmacy,please call or whatsapp +255767650213 for pharmaceutical services.
    Follow our blog www.bajileson.blogspot.com for articles and infographics on medicines!

    Picha|Mchina wa geita akamatwa

    Raia wa China, Leo Swi akikamatwa kwa tuhuma za kumtesa mfanyakazi wa mfanyakazi wa mgodi wa madini wa Nyamahuna, Geita, Masanja Shokaa baada ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba kutembelea mgodi huo.
    Source:Mwananchi
    Thursday, 28 July 2016

    BBC Swahili|Wanasayansi Wagundua Dawa Kwenye Pua Ya Binaadamu

    Wanasayansi nchini Ujerumani wanasema wamegundua kwamba kuna chembechembe hai kwenye pua ya mwanadamu ambayo inaweza kutumia kuua viini hatari.
    Dawa nyingi za kuua viini vinavyosababisha maradhi hutolewa kutoka kwenye wanaoishi kwenye mchanga.
    Lakini kutokana na hali kwamba viini vinavyosababisha magonjwa mengi vimeanza kuwa sugu na kutosikia dawa, wanasayansi wamekuwa wakitafuta njia nyingine za kupata dawa mpya.
    Ripoti ya vipimo imebaini katika jarida la asili kwamba dawa aina ya Lugdunin, inaweza kutibu maambukizi ya maradhi yasiyosikia dawa.
    Watafiti katika chuo kikuu cha Tubingen nchini Ujerumani, waliogundua chembe hizo wanasema kuwa mwili wa binaadamu ni chanzo cha dawa mpya ambazo bado hazijatumiwa.
    Dawa ya mwisho kugunduliwa katika mwili wa binadamu ilipatikana mwaka 1980.
    Source:BBC SWAHILI

    Alazwa Bugando Mwaka Mzima Kwa kunywa Kemikali

    ALAZWA HOSPITALI MWAKA MZIMA BAADA YA KUNYWA CAUSTIC SODA
    ** Afya ya msichana wa miaka 17 ambaye utumbo wake na koromeo viliharibika vibaya baada ya kunywa chemikali aina ya caustic soda akidhani ni maji safi na salama ya kunywa inaendelea kuzorota katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando (BMC) mkoani Mwanza alikolazwa kwa zaidi ya mwaka mmoja kwa ajili ya matibabu.
    Hawezi kula chakula kwa njia ya kawaida kwani mfumo wake wa chakula umefungwa, licha ya kufanyiwa upasuaji mara kadhaa tangu alipofikishwa BMC Aprili mwaka jana.
    Source na ingia hapa kupata stori kamili http://www.mwananchi.co.tz/habari/Alazwa-hospitali-mwaka-mzima-baada-ya-kunywa-caustic-soda/1597578-3319698-6yqqn0z/index.html

    Mzunguko wa hedhi na njia salama ya uzazi wa mpango kwa kutumia kalenda

    Wanawake wengi wamekuwa na malalamiko juu ya utumiaji wa vidonge au sindano kuzuia mimba au kupanga uzazi!Kwa ufupi njia ya kalenda ni njia iliyo salama zaidi kiafya..
    Picha niliyoweka ni kwa ufupi utakavyoweza kuhesabu au kujua siku zipi ni za hatari na zipi ni salama..kwa mfano kwenye nyekundu ni siku ambazo utakuwa hedhi na utaanza kuhesabu siku ya kwanza tangu ulipoanza na utaendelea na mzunguko kama unavyonyesha katika picha..sehemu iliyochorwa mtoto ni siku ambazo ukifanya tendo la ndoa basi ni siku ambazo utapata ujauzito...Kuwa makini kwa kufuata idadi ya siku tangu umeanza bleed siku ya kwanza..Siku njema!
    Wednesday, 27 July 2016

    Buswelu pharmacy

    For services and medicine use consultation please call +255767650213
    Follow our blog www.bajileson.blogspot.com for news,pictures and medical articles.

    Upungufu wa damu kipindi cha ujauzito

    UPUNGUFU WA DAMU KIPINDI CHA UJAUZITO (ANAEMIA IN PREGNACY)

    Upungufu wa damu (anaemia) hutafsiriwa kama kupungua kwa kiwango cha hemoglobin katika damu damu chini ya kiwango kinachokubalika kiafya. Kiwango cha kawaida cha haemoglobin (Hb) katika mwili wa binadamu ni kati ya gramu 12 mpaka 14 kwa kila mililita ya damu. Hata hivyo shirika la afya duniani (WHO) linatambua kiwango cha mpaka 11gm/mililita kuwa cha kawaida kwa mama mjamzito. Hivyo basi mjamzito mwenye kiwango chochote cha haemoglobin chini ya 11 gm/mililita hutafsiriwa kuwa na upungufu wa damu.

    Hata hivyo nchi nyingi hasa zinazoendelea hutambua kiwango cha mpaka gramu 10 kwa mililita kuwa ni upungufu wa damu kwa mjamzito.Kwa mjamzito anayehudhuria kliniki kwa mara ya kwanza, upungufu wa damu kipindi cha ujauzito humaanisha kiwango cha hemoglobin chini ya <11.0 g/dL, na mimba inapofikisha wiki 28 upungufu wa damu hutambuliwa iwapo hemoglobin itashuka na kuwa chini ya 10.5 g/dL.Kwa kuzingatia hilo, mama mjamzito hushauriwa kupima wingi wa damu siku anapohudhuria kliniki kwa mara ya kwanza na pindi mimba inapofikisha wiki 28.

    Viwango vya Anaemia
    Upungufu wa damu unaweza kugawanywa katika viwango vikuu vinne, yaani upungufu wa damu wa kawaida (mild anaemia) ambao ni kati ya 9-11 gm/ml, upungufu wa damu wa kati (moderate anaemia) ambao ni kati ya 7-9 gm/ml, upungufu wa damu mkali (severe anaemia) ambao ni kati ya 4-7 gm/ml na upungufu wa damu mkali zaidi (very severe anaemia) ambao ni chini ya 4gm/ml.

    Mzunguko wa madini ya chuma mwilini
    Kwa kawaida mwili wa mwanamke huifadhi gramu 3.5 mpaka 4.5 za madini ya chuma. Asilimia 75 huifadhiwa kama hemoglobin katika chembe damu nyekundu, asilimia 20 kama ferritin katika mifupa na asilimia 5 inayobaki huifadhiwa katika misuli na vimengenyo vingine vya mwili.

    Wanawake wasio wajawazito hupoteza karibu gramu 1 za madini ya chuma kutoka katika seli za mwili zinazokufa kila siku na gramu 1 zaidi kila siku wanayokuwa kwenye hedhi.

    Ukubwa wa tatizo
    Upungufu wa damu kipindi cha ujauzito ni tatizo linalowakumba kina mama wajawazito wengi sana, siyo tu Tanzania bali nchi nyingi zinazoendelea. Inakisikiwa kuwa karibu theluthi moja ya wajawazito katika miezi mitatu ya mwisho ya ujauzito hukumbwa na tatizo hili.

    Kwa mujibu wa WHO, inakadiriwa kuwa karibu asilimia 56 ya wajawazito huko kusini mashariki ya Asia hukumbwa na tatizo hili. Kwa hapa Tanzania, hakuna takwimu sahihi kuhusu tatizo hili. Sehemu nyingine duniani, inakadiriwa kuwa karibu asilimia 4-16 ya vifo vinavyotokana na ujauzito husababishwa na upungufu wa damu. Aidha upungufu wa damu wakati wa ujauzito huongeza uwezekano wa madhara kwa mtoto ikiwemo kifo.
    Chanzo cha upungufu wa damu wakati wa ujauzito
    Kipindi cha ujauzito huambatana na mabadiliko mbalimbali ya mwili. Moja ya mabadiliko hayo ni ongezeko la maji (plasma volume) katika mzunguko wa damu. Katika hali hii, pamoja na kwamba kiasi cha damu huonekana kuongezeka, kiwango cha hemoglobini hupungua mpaka kufikia 11.5mg/dl.
    Karibu asilimia 85 ya anaemia wakati wa ujauzito husababishwa na upungufu wa madini ya chuma mwilini. Upungufu wa madini ya chuma unaweza kusababishwa na kula chakula chenye kiasi kidogo cha madini haya au mwili wa mjamzito kushindwa kutunza madini ya chuma ya kutosha kutokana na ama mimba zilizopita au kupoteza kiasi kingi wakati wa hedhi kabla ya kushika mimba.

    Vyanzo vingine ni pamoja na
    Upungufu wa folic acid
    Ugonjwa wa sickle cell
    Lishe duni kabla na wakati wa ujauzito
    Kupoteza damu kwa sababu ya kuumia au kuwa na minyoo (hookworms)
    Ugonjwa wa malaria wakati wa ujauzito
    Ugonjwa wa chembe damu nyekundu ujulikanao kama beta thalassaemia. Ugonjwa huu huwapata zaidi watu wanaoishi Asia ya kusini, Ulaya ya kusini na Afrika.
    Upungufu wa vitamin B12
    Ugonjwa sugu wa kuvunjika chembe damu nyekundu (chronic haemolysis) kama vile ugonjwa kurithi wa chembe damu nyekundu (hereditary spherocytosis
    Ugonjwa wa kupoteza hemoglobin kupitia mkojo (paroxysmal nocturnal hemoglobinuria)
    Saratani ya damu (leukemia)
    Matatizo ya kupoteza damu kwenye njia ya chakula (gastrointestinal bleeding)
    Matatizo katika utumbo hasa wakati wa ujauzito.

    Vihatarishi vya tatizo hili
    Masuala ya kijamii kama vile umri wa mjamzito, kiwango chake cha elimu na uelewa kuhusu afya yake, kama ana mwenza wa kumsaidia kiuchumi, makazi anayoishi vinaweza kuchangia mjamzito kupata upungufu wa damu
    Vihatarishi vingine ni vile vinavyohusu masuala ya uzazi kama vile idadi ya mimba zilizotanguli (waliowahi kuzaa wana hatari ya kupata anaemia kuliko wanaopata mimba kwa mara ya kwanza), kuwa na mimba ya mapacha na kuwa na historia ya kuzaa mtoto njiti
    Vihatarishi vingine vinahusu tabia za mjamzito kama vile uvutaji sigara, unywaji wa pombe na kutohudhuria kliniki wakati wa ujauzito

    Pia kuwa na magonjwa kama vile kisukari, magonjwa ya figo, pamoja na shinikizo sugu la damu
    Madhara ya upungufu wa damu kwa mama na mtoto

    Sehemu nyingine duniani, inakadiriwa kuwa karibu asilimia 4-16 ya vifo vinavyotokana na ujauzito husababishwa na upungufu wa damu. Aidha upungufu wa damu wakati wa ujauzito huongeza uwezekano wa madhara kwa mama na mtoto ikiwemo kifo. Madhara haya ni pamoja na
    Madhara kwa mama kipindi cha ujauzito: kukonda au kuongezeka uzito kwa kiasi kidogo sana, kuhisi uchungu kabla ya muda, kondo la nyuma kutunga pasipostahili, shinikizo la damu wakati wa ujauzito, na chupa kupasuka kabla ya wakati.Madhara kwa mama wakati wa kujifungua: kupatwa na uchungu usioeleweka na usio wa kawaida, mtoto kuvuja damu ndani kwa ndani, kupatwa na shock, hatari ya ganzi (anesthesia risk) kwa anayefanyiwa upasuaji, na moyo kushindwa kufanya kazi.

    Madhara kwa mama baada ya kujifungua: maambukizi baada ya kujifungua, kizazi kushindwa kurudi katika hali ya kawaida au damu kuganda kwenye mishipa.Madhara kwa mimba na mtoto atakayezaliwa: Madhara ni pamoja na mtoto kuzaliwa njiti, mtoto kuzaliwa na uzito mdogo, mtoto kuwa na score ndogo (poor Apgar score), mtoto kuzaliwa akiwa amechoka (fetal distress), na upungufu wa damu kwa mtoto
    Watoto wanaozaliwa wakiwa na upungufu wa damu hukua kwa tabu, huwa na maendeleo duni ya kiakili na kimatendo (poorer intellectual developmental milestones), uwezekano mkubwa wa kuwa na kasoro mwilini na hata kifo. Kasoro hizo ni pamoja na matatizo ya magonjwa ya moyo ya kuzaliwa nayo (congenital heart diseases)

    Mjamzito mwenye upungufu wa damu wa kawaida mara nyingi anaweza asioneshe dalili zozote. Hata hivyo iwapo upungufu ni mkubwa, dalili za awali ni pamoja na uchovu wa mara kwa mara na kupumua kwa shida, kukosa hamu ya kula, mapigo ya moyo kwenda kasi, na kuchafuka kwa tumbo.Wakati wa uchunguzi mjamzito anaweza kuonekana mweupe kuliko kawaida hasa sehemu za viganjani, kucha za vidoleni, ulimi, au macho. Anaweza pia kuwa na dalili za kuvimba miguu.

    Dalili nyingine ni kama zilivyoelezwa katika makala iliyopita ya upungufu wa damu.

    Vipimo na uchunguzi
    Uchunguzi wa upungufu wa damu hufanywa kuwa kupima kiasi cha haemoglobin pamoja kufanya kipimo kingine cha damu kijulikanacho kama peripheral smear.

    Vipimo vingine vya maabara ni pamoja na kipimo cha kufahamu uwezo wa kuhifadhi madini ya chuma yaani total iron binding capacity (TIBC), kiasi cha feritinkatika damu, kiasi cha folic acid. Katika mazingira mengine kipimo cha kuchukua sehemu ya supu ya mifupa na kuichunguza maabara yaani bone marrow biopsykinaweza kufanywa. Hata hivyo hivi si vipimo vinavyofanywa mara kwa mara.

    Matibabu
    Mama mjamzito huitaji miligramu 2 mpaka 4.8 za madini ya chuma kila siku. Ili aweze kupata kiasi hiki, inampasa kula kati ya miligramu 20 mpaka 48 za madini ya chuma. Kwa jamii ambayo upatikanaji wa vyakula vyenye madini hayo ni wa shida, suala hili linaweza kuwa gumu sana kutekelezeka, ndiyo maana Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii imeweka mpango maalum wa kuwapa wajawazito wanaohudhuria kliniki madini ya chuma na folic acid ili kufidia pengo hilo.

    Vidonge vya madini ya chuma ni salama, nafuu na njia makini ya kuongeza na kurekebisha upungufu wa damu mwilini. Kwa wajawazito ambao hawawezi kunywa, kwa sababu yeyote ile, njia ya sindano inaweza pia kutumika.

    Wajawazito wanashauriwa kutumia miligramu 60 za madini ya chuma (ferrous sulphate) na 500mg za folic acid kila siku, ambapo utaratibu huu huendelea kwa miezi mitatu mpaka sita ili kuongeza hifadhi ya madini ya chuma mwilini, hata kama kiwango kinachotakiwa kitakuwa kimefikiwa.
    Utumiaji wa vidonge vya madini ya chuma na baadhi ya vyakula: Kuna baadhi ya vyakula kama vile chai ya rangi ambavyo vikiliwa wakati mjamzito amekunywa vidonge vya madini ya chuma vinaweza kupunguza unyonyaji wake katika utumbo. Kwa upande mwingine baadhi ya vyakula vyenye vitamini C kama vile matunda ya jamii ya machungwa huongeza uwezo wa utumbo kunyonya madini ya chuma mwilini.

    Vyakula vya kuongeza damu: Pamoja na mkakati huo, wajawazito hushauriwa pia kula vyakula vyenye madini ya chuma kwa wingi kama vile nyama, maini, mayai, samaki, mimea jamii ya kunde, maharage makavu, mboga za majani, matembele, na mikate iliyoongezwa madini ya chuma.
    Matibabu ya upungufu wa damu mkali kwa wajawazito walio katika wiki za mwisho (baada ya wiki ya 32): Wagonjwa wa kundi hili hutibiwa hospitali. Wengi wanaweza pia kuwa na dalili za matatizo ya moyo, hivyo wanapaswa kulazwa na kupumzika kitandani, na wakati fulani kuongezewa hewa ya oksijeni. Pamoja na kutibiwa matatizo ya moyo, huongezewa pia damu (packed red cells) kwa vile vidonge vya madini ya chuma havitafaa kurekebisha tatizo hili kwa haraka kabla ya muda wa kujifungua kufika.
    Matibabu ya maradhi mengine: kwa mazingira yetu, magonjwa kama malaria na minyoo huchangia kwa kiasi kikubwa kutokea kwa upungufu wa damu kwa wajawazito, hivyo basi magonjwa haya hayana budi kutibiwa kikamilifu ili yasilete madhara kwa mjamzito. Wajawazito wanaoishi maeneo yenye malaria kwa wingi hupewa dawa za SP kwa ajili ya kuzuia malaria
    Source:Jamii forums

    Makonda abaini ufisadi machinga complex,Dar

    TAARIFA YA MRADI WA MACHINGA COMPLEX
    1.0 Utangulizi
    Mnamo tarehe 19 Aprili, 2016 ofisi yangu ya mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam ilipokea barua ya agizo la waziri wa nchi TAMISEMI juu ya kusimamia uendeshaji wa mradi wa Machinga Complex. Ambapo katika kutekeleza agizo hilo nilichukua hatua ya kwanza na ya muhimu ya kuupitia mkataba wote wa mradi huu ikiwa ni pamoja na kufanya tathmini ya haki na wajibu wa pande mbili zilizohusika kwa maana ya Halmashauri ya Jiji na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF).
    Kimsingi, tathmini yangu ya mkataba ililenga kubainisha na kujiridhisha juu ya mambo sita yafuatayo; aina ya jengo lililotarajiwa kujengwa, usimamizi wa fedha za mkopo, usimamizi wa ujenzi wa mradi, gharama za mradi, utaratibu wa urejeshaji wa deni na kiwango cha riba kilichoainishwa. Ikukumbukwe tu kwamba, wakati halmashauri ya jiji ikikabidhiwa mradi siku ya kwanza ilikuwa tayari inadaiwa kiasi cha bilioni 19.7 huku mpaka Machi mwaka huu deni lilishafikia kiasi cha bilioni 38 za kitanzania, kutokea kwenye mkopo wa bilioni 12.7
    2.0 Uchunguzi
    Baada ya kupitia kwa umakini mkataba mzima na kukagua mradi wenyewe, zoezi ambalo lilihusisha kulinganisha kati ya kilichofanyika baada ya mradi kukamilika na taarifa ya upembuzi yakinifu (feasibility study) uliofanyika kabla ya kuanza utekelezaji wa mradi nimebaini yafuatayo;
    2.1 Ukubwa halisi wa jengo
    Nimebaini kwamba majengo ya sasa ya machinga complex hayakujengwa kwa ukubwa sawa na ule ambao Halmashauri ya Jiji na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) walikubaliana kwenye mkataba na kupitia kifungu cha 1.1 cha barua ya makabidhiano kinachoeleza kwamba jengo lililokabidhiwa lina sehemu yenye ghorofa 5 na ghorofa 6 ili liweze kumudu idadi ya machinga wasiopungua 10,000 wakati hali halisi baada ya kutembelea jengo hilo ni kwamba jengo lina ghorofa 4 zinazobeba machinga 4,000 tu.                                                                                                                                      Kwahiyo, pamoja na kwamba barua ya makabidhiano ilisainiwa na pande zote mbili licha ya ukweli kuwa maelezo ya jengo yalikuwa tofauti na jengo lenyewe.
    2.2 Usimamizi wa fedha za Mkopo
    Kwenye usimamizi wa fedha za Mkopo, Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ambaye ni mkopaji hakuhusika na usimamizi wa fedha za mkopo, hivyo mkopeshaji hakuwa na udhibitisho wa gharama halisi, jambo ambalo si tu limefanya mkopaji kutojua gharama halisi za jengo bali pia kulipokea likiwa limechelewa na likiwa halina ukubwa ulioelezwa kwenye mkataba. Kimsingi, haya yote yanazaliwa na maelekezo ya kifungu namba 4.1 kinachoeleza kwamba, mkopeshaji kusimamia mradi kuanzia hatua ya usanifu hadi kukamilika kwake ikiwa ni pamoja na kufanya malipo moja kwa moja kwa mkandarasi na mshauri wa mradi, kwa maneno mengine pia ni kwamba kifungu hiki kinakinzana na vifungu namba 2.1, 2.2, 10.1 na 11.1 vya mkataba huohuo ambavyo vinaelekeza kwamba mkopeshaji (NSSF) atatakiwa kutoa fedha kwa mkopaji (Halmashauri ya Jiji) kwa ajili ya kugharamia mradi pekee na kuusimamia kama ulivyokubalika kwenye mkataba.
    2.3 Kuhusu gharama za mradi
    Nimebaini kuwa fedha za mkopo ziliongezeka toka shilingi bilioni 12.14 za kwenye mkataba na kufikia bilioni 12.7 ikiwa ni nyongeza ya shilingi milioni 560, nyongeza ambayo ilifanyika bila makubaliano yoyote kati ya mkopeshaji na mkopaji, hali ambayo haimtendei haki mkopaji. Kwa faida tu ya wanadar es salaam na watanzania wenzangu ni kwamba, halmashauri ya jiji ilitiliana saini ya makubaliano na shirika la hifadhi ya jamii (NSSF) ya mkataba ambao unalenga kuipatia halmashauri ya jiji mkopo wa bilioni 10 kwa ajili ya kutekeleza mradi huu ingawa baada ya muda kidogo mkopeshaji (NSSF) alisema kuwa bilioni 10 na hivyo kufanya marekebisho ya mkataba na kuongeza mkopo wa bilioni 2.14
    2.4 Urejeshaji wa deni
    Suala la urejeshaji wa mkopo unazua utata pale mkataba unapoainisha kuwa, mkopaji ataanza kulipa marejesho ya deni kuanzia tarehe 31 Desemba, 2008 tarehe ambayo mradi ulikuwa unatarajiwa kuwa tayari umeanza lakini mkopeshaji (NSSF) alikuwa hajamaliza ujenzi, na cha ajabu mkopaji (Halmashauri ya Jiji) alitakiwa kuanza kulipa deni hata kabla ya muda wa grace period kuisha wakati jengo likiwa bado lipo mikononi mwa mkopeshaji ambaye alijitwisha jukumu la ujenzi huku akiwa bado akang’ang’ania kulipwa riba.
    mara tu tarehe hiyo ilipofika hata kama mpokeshaji mwenyewe alikuwa bado hajakamilisha ujenzi huku akidai pesa ya riba.
    Uwezo wa Mradi
    Uwezo wa jengo hilo  lililopo hata kama litafanya kazi kwa uwezo wake wote kwa maana ya kujaza nafasi zote zilizopo ni kasi cha sh124,796,666.666 kwa mwezi ambazo ni sawa na kiasi cha sh1,497,560,000  kwa mwaka. Pungufu ya 60% ya lengo la Mradi kama ilivyokuwa kwenye upembuzi yakinifu.
    3.0 Mapendekezo
    3.1 Baada ya uchunguzi huu ulionifanya kuamini mambo makubwa matano niliyoyaainisha hapo chini na ambayo yameniongoza kutoa mapendekezo ya hatua za kuchukua;-
    •    Deni halilipiki – ukweli ni kwamba, ukizingatia kiasi cha pesa kinachodaiwa kutoka kwa halmashauri ya Jiji ambacho mpaka sasa ni zaidi ya bilioni 38 utagundua kuwa, halmashauri haiwezi kulipa deni hilo. Ikilinganishwa na uwezo wa jengo hilo deni hili litalipwa baada ya miaka isiyopungua 24
    •    Mkataba wote huu ni wa hovyo na haukupaswa kusainiwa hata kidogo.
    •    Kitendo cha kusaini mkataba huu ni hakika na bayana kuwa rushwa ilitumika pande zote mbili, kwa maana haiwezekani ukaacha taaluma yako kwa kiwango hicho cha kutoona udhaifu huu wa wazi wa mkataba huu kama hujapofushwa macho na rushwa.
    •    Mkataba huu hauna tija kwa upande wowote ule: sio NSSF kwasababu halmashauri ya Jiji hawana uwezo wa kulipa deni, wala sio kwa Jiji lenyewe kwani halina uwezo wa kutekeleza mkataba kwa kufanya malipo yanayotakiwa na hauna faida vilevile kwa machinga kwa sababu gharama ya kupanga ni kubwa.
    3.2 Mapendekezo
    1.    Kuvunjwa kwa mkataba na NSSF kuchukua eneo lao, kwa makubalino ya kwamba, Halmashauri ya Jiji walipwe kodi ya ardhi jambo ambalo linaweza kufanyika kwa urahisi kupitia NSSF na halmashauri ya Jiji kumiliki hisa kwa pamoja.
    2.    Au NSSF wakabidhi jengo kwa halmashauri ya Jiji, lakini wakae na kukubaliana upya na hivyo kuandika mkataba tofauti na ule wa mwanzo.
    3.    Mwisho, wahusika wote wa pande zote mbili wachukuliwe hatua kwani hatuwezi kutumia fedha za mifuko za hifadhi ya jamii ambazo ni fedha za wanyonge wa taifa hili kwa faida ya wachache waliotanguliza ubinafsi,

    Imetolewa na:Paul Makonda
    Mkuu wa Mkoa – Dar es Salaam

    Tuesday, 26 July 2016

    Role of a pharmacist

    Mojawapo ya majukumu ya msingi ya mfamasia ni kutunza dawa,kuhakikisha matumizi sahihi ya dawa,kuhakikisha ubora wa dawa na upatikanaji wa dawa wakati wote,kushirikiana na wataalamu wengine kuhakikisha usahihi wa tiba,kuelimisha jamii juu ya madhara ya dawa n.k

    Buswelu pharmacy inside look

    For more details about our services and medicines use consultation please call or whatsapp +255767650213
    We are located at Buswelu center,Ilemela district in Mwanza region.

    Je,Ni salama kutumia dawa iliyokwisha muda wake?

    Nini maana ya expired medicines?

    Ni siku ya mwisho ambapo mtengenezaji wa dawa (Manufacturer)  amekuhakikishia (Gurantee) usalama na ufanyaji kazi bora wa dawa husika (Safety and Potency).

    Mara nyingi huwekwa kwenye makasha (Containers) ya dawa kama alama (Labels) na hata vyeti vya dawa (Prescriptions). Pia tarehe ya kikomo ya dawa (Expiration date) huwa inapimwa kupitia jaribio la  uimara (Stability testing) chini ya njia bora za uzalishaji (Good manufacturing practices) zilizowekwa na mamlaka zinazosimamia watengeza dawa kwa nchi husika mfano TFDA kwa Tanzania.

    Kwa ufupi ni kuwa dawa inapotengezwa, muda ambao dawa itakuwa na nguvu na kuanza kupoteza nguvu hupimwa (Shelf life). Mtengeneza dawa hufanya hivyo kukuhakishia kuwa dawa inapotumika ndani ya huo muda wa kuwa na nguvu itafanya kazi kwa kiwango cha juu cha ubora na usalama wake (Potency and safety)

    Je, Dawa huisha nguvu na usalama mara tu pale tarehe ya kikomo ilivyowekwa?

    Tafiti nyingi zimeonyesha kuwa bado dawa nyingi zina ubora na usalama hata baada ya kupita tarehe ya kikomo cha dawa kama ilivyoandikwa kwenye kasha hasa dawa zenye umbile la vidonge na capsules kwani ni imara (Stable). Lakini mara nyingi ni ngumu kuweza kujua kuwa ni siku gani hasa ubora au usalama huo wa dawa umekwisha kabisaa.

    Madhara

    Kutumia Dawa iliyokwisha nguvu na usalama (Sub potent medicines) ni hatari kwa afya. Kwani inaweza kuleta madhara kama usugu wa vijidudu vya magonjwa hasa bakteria na hata kifo. Dawa zinazotolewa kwa njia ya sindano pia si salama kuzitumia baada ya kuisha  muda kwani zinaweza kusababisha madhara makubwa kwani vijidudu (kama fungasi na bakteria) huweza kuota kwenye dawa hizo zenye asili ya majimaji au powder na kuleta madhara makubwa zaidi endapo wataingia mwilini

    Dawa za kutibu kisukari kwa mfano huwa ni rahisi kupungua kiwango cha kutibu (Susceptible to degration) mara tu baada ya siku au tarehe ya kikomo.

    Hata hivyo wataalamu wanashauri utunzaji ulio bora wa dawa (Storage) unaweza kusaidia kuendelea kwa nguvu ya dawa (Therapeutic effect) hata baada ya tarehe ya mwisho ya kutumia. Dawa mara nyingi hubaki na uimara wake inapotunzwa kwenye ukavu, sehemu yenye ubaridi baridi na mbali na joto au mwanga wa jua.

    Baadhi ya dawa nyingine kama antibiotiki inayoitwa Tetracycline hugeuka kuwa sumu baada ya muda wake wa matumizi kuisha na huweza kusababisha matatizo kwenye figo

    Je, Ni sawa kwa mgonjwa kutumia dawa iliyofikia tarehe ya kikomo ?

    Ni vyema kubadili dawa pindi tu unapogundua imefikia tarehe ya kikomo. Japokuwa hakuna uthibitisho wa moja kwa moja wa kwamba si salama kunywa dawa iliyofika kikomo, lakini kwa magonjwa yanayohatarisha maisha (chronic and life threatening diseases) kama ya moyo, kifafa, allergy ni ushauri uliowazi kabisa si vyema kutumia dawa hizo baada ya tarehe ya kufika kikomo (Expired date). Kwa ufupi ni Kwamba ni nani ambaye yuko tayari kuhatarisha maisha au afya yake. Chukua tahadhari!!!

    Cha kujifunza

    Tarehe ya mwisho ya kikomo cha dawa imewekwa kama kipimo (Conservative measure) ili kukuhakishia uinatumia dawa iliyo na uimara wa kufanya kazi (Highest potency).

    Wakati unaumwa, unachofikiria kwa haraka ni kupona mara moja. Kutumia kitu ambacho una kiamini kama tiba ndio jambo la msingi kuliko kutumia kitu chenye kukuletea mashaka.

    Mbali ya kuwa dawa nyingi zimewekewa alama za muda wa kuisha, lakini utunzaji wa dawa mzuri bado ni njia bora Zaidi ya kuhakikisha uimara wa dawa hiyo (Effectiveness)

    Asante.

    By Mafamasia, Michael Bajile
    January 2015

    Madhara yatokanayo na vipodozi vyenye sumu au feki

    Kwa dunia ya sasa, ni jambo la kawaida sana watu kutumia vipodozi ili waweze kuwa na muonekano wanaotaka!Lakini wimbi la watumiaji limekua likiongezeka siku hadi siku na hii ni kutokana na mabadiliko au mfumo wa maisha ya kisasa..Watumiaji wengi ni akina dada au vijana kati ya miaka 16 hadi 38.Pia kwa miaka ya hivi karibuni kuna wimbi kubwa la vijana walioathirika na utumiaji wa vipodozi visivyo salama na wengi bado hawajui ni vipodozi vipi tunasema ni salama na vingine si salama

    Kutokana na wimbi hili la vijana wengi kuwa na madhara kwa kutokujua au wengine hata kwa kujua, nimeamua kukuletea  makala hii fupi lengo hasa ni kuweza kukusaidia/kuisaidia jamii hii hasa wale wasiofahamu aina za vipodozi vinavyoweza kuleta madhara. Lakini kabla hatujayazungumzia madhara, tuangazie kwa pamoja maana ya kipodozi!

    Nini maana ya vipodozi?

    Sheria ya mamlaka ya chakula, dawa na vipodozi yaani “Tanzania food, drugs and cosmetics act” ya mwaka 2003, inafafanua kuwa kipodozi ni kitu chochote kilichodhamiriwa kutumiwa kwa kupaka, kujimwagia, kujifukisha, kujipulizia au namna nyingine kwenye mwili wabinadamu kwa lengo la kujitakatisha, kujiremba au kuongeza mvuto au kubadilisha muonekano pamoja na mambo mengine yenye malengo kama hayo.

    Ni ukweli usiopingika kuwa vipodozi vimetengenezwa kwa kemikali au viambata ambavyo baadhi si salama na vingine ni salama iwapo vitatumiwa katika mwili wa binadamu.

    Makala hii fupi kama nilivyotangulia kusema itakuwezesha msomaji kujua baadhi ya kemikali zinazoweza kukuletea madhara pindi utakoputumia vipodozi.

    Mamlaka ya chakula na dawa ni mamlaka iliyoanzishwa kisheria na lengo kuu ni kusimamia ubora na usalama wa bidhaa kuanzia zinapotengezwa, kusafirishwa, kusambazwa na kutumiwa na wateja.

     Kutokana na hilo basi, mamlaka hii pia imekuwa ikisaidia kwa kiasi kikubwa kudhibiti bidhaa ambazo si salama kwa watumiaji hasa vipodozi na dawa feki au zilizokatazwa.

    Tangu kuanza kwa udhibiti, aina 250 za vipodozi zimesha pigwa marufuku kwani zina viambata ambavyo si salama kwa matumizi. Idadi hii inaweza kuongezeka kutokana na matokeo ya chunguzi mbalimbali.

    Mfano wa vipodozi au cream zilizopigwa marufuku ni kama carolite, mikorogo au kama picha hapo inavyoonyesha. Hakika kama unavyoviona ni vipodozi tunavyovijua na wengi bado tukiendeelea kuvitumia.

     Ni viambata vipi au kemikali zipi tunasema si salama?

    Kemikali hizo zinazotajwa ni kama ifuatavyo:

    Biothionol, Hexachlorophene, Zebaki au mercury, Vinyl chloride, zirconium, Halogeneted salicynilides, chloroquinone, steroids, choloroform, methylene chloride na chlorofluorocarbon propellants.

    Madhara

    ·         Kupata mzio wa ngozi na athari kwenye ngozi ikiwa itapata mwanga wa jua kwa

    ·         Baadhi  hupenya kwenye ngozi na kuingia kwenye mishipa ya fahamu na kusababisha ugonjwa wa mishipa ya fahamu hasa kichwa

    ·         kwa wamama wajawazito huweza kuathiri ubongo wa watoto wao

    ·         Ngozi kuwa laini na kusababisha magonjwa kama fangasi au maambukizi ya vimelea vingine

    ·         Zebaki au mercury husababisha madhara ya ngozi, ubongo, figo na viungo mbalimbali.

    ·         Ngozi kuwa laini,mabakabaka, muwasho na mzio wa ngozi.

    ·         Zebaki pia inaweza kusababisha upofu, uziwi, upotevu wa fahamu wa mara kwa mara.

    ·         Kansa

    ·         Kwa viambata vyenye steroids vikitumika kwa muda mrefu husababisha madhara kama ugonjwa wa ngozi na kutokwa na chunusi kubwa, ngozi kuwa nyembamba na laini na endapo mtu atapata jeraha au kufanyiwa upasuaji kidonda hakitapona, pia husababisha magonjwa ya moyo.

    Jitihada za mamlaka ya chakula na dawa

    Mamlaka imejitahidi kwa kiasi kikubwa kupambana na vipodozi hivi feki lakini bado inakabliwa na changamoto kwa mfano wa rasilimali watu, si rahisi wafanyakazi wa mamlaka kuwa kila eneo linalouzwa vipodozi. Pia vipodozi hivi vimekuwa vikiingizwa nchini kupitia katika mipaka isiyo rasmi au njia za panya na walanguzi au wafanya biashara wasio na mapenzi mema kwa afya yako. Pia uelewa wa jamii bado uko chini sana kuhusiana na madhara au matumizi ya viambata vyenye madhara.

    Cha kujifunza

    Hivyo  basi ni jukumu letu sote kama wadau kuweza kusaidiana kuelimisha jamii au kuisadia mamlaka kwa kutoa taarifa za watu wanaovunja sheria za mamlaka kwa kuuza vipodozi vyenye madhara au kemikali tajwa ili waweze kuchukuliwa hatua na hatimaye kuweza kulinda afya za watanzania na taifa kwa ujumla.Pia ni jukumu la watumiaji kuchukua tahadhari kwa kutotumia bidhaa zilizokatazwa na mamlaka kwani ni hatari kwa ustawi wa afya zetu.

    Ni matumaini yangu msomaji umeweza kuzifahamu kemikali zenye madhara,sina la ziada kwa leo na nina amini umeweza kujifunza mengi kuhusiana na madhara yatokanayo na viambata vyenye sumu kwenye vipodozi.

    Imeandaliwa na  Mfamasia, Michael Bajile.

    18th January 2015

    Monday, 25 July 2016

    Picha 7: DC Korogwe ashiriki ujenzi wa zahanati, apanga kukamilisha ndani ya siku 30


    Umbali mrefu wa kufuata huduma ya afya umemfanya Mkuu wa wilaya ya Korogwe,Gabriel Robert kushirikiana na wananchi wa kijiji cha Mwenga Tarafa ya Mombo kuanza ujenzi wa zahanati ambayo wamelenga kujenga zahanati yenye viwango vya ubora na vigezo vyote vya kitaalamu ndani siku 30 kuanzia leo.
    IMG-20160723-WA0014
    Mkuu wa wilaya ya Korogwe, Gabriel Robert akishiriki kuchimba msingi wa ujenzi wa zahanani kijiji cha mwenga
    IMG-20160723-WA0004

    IMG-20160723-WA0040
    DC Korogwe, Gabriel Robert
    IMG-20160723-WA0006

    IMG-20160723-WA0007

    IMG-20160723-WA0009
    DC Korogwe, Gabriel Robert
    IMG-20160723-WA0021
    Wananchi wa kijiji cha Mwenga waliojitokeza kusaidia ujenzi wa zahanati

    ‘Hata nitakapotangulia mbele ya haki niiache Tanzania ikiwa na amani’ -Rais JPM


    July 25 2016 Serikali ya Tanzania imefanya  maadhimisho ya siku ya mashujaaambapo mgeni rasmi alikuwa ni Rais John Pombe Magufuli alikuwa mgeni rasmi katika maadhimisho hayo yaloiyofanyika kitaifa Dodoma.
    Katika hotuba yake Rais Magufuli hakuacha kusisitizia suala la amani katika taifa huku akiwataka watanzania wote kwa pamoja kuhakikisha wanailinda na kuidumisha.
    Tunapoadhimisha siku ya mashujaa, tunawakumbuka wote waliotoa uhai wao kuhakikisha nchi inakuwa na amani, hawa mashujaa wetu waliofariki hawakujali dini, vyama wala makabila yao, tunapowakumbuka tuilinde amani‘ –Rais Magufuli
    Niviombe vyama vyote wawe wahubiri wa amani kwakuwa  maendeleo ya nchi yetu yatapatikana kama tutailinda amani tuliyonayo, hata nitakapotangulia mbele ya haki niiache Tanzania ikiwa na amani’ –Rais Magufuli
    Lakini pia Rais Magufuli hakulikalia kimya hili la mpango wa Serikali kuhamishia makazi yake Dodoma ambapo amesema …>>>’Haiwezekani Serikali ninayoiyongoza ishindwe kuhamia Dodoma, leo tunamkumbuka pia baba wa taifa aliyesema makao makuu yawe Dodoma, sisi hatuwezi kupinga hatua hiyo‘ –Rais Magufuli
    Friday, 22 July 2016

    SIDE EFFECTS ZA ASPIRIN

    Aspirin: side effects ASPIRIN:
    Asthma
    Salicyalism
    Peptic ulcer disease/ Phosphorylation-oxidation uncoupling/ PPH/ Platelet disaggregation/ Premature closure of PDA
    Intestinal blood loss
    Reye's syndrome
    Idiosyncracy
    Noise (tinnitus)

    MATUMIZI YA ANTIBIOTIC MAARUFU (COMMON ANTBIOTICS) KWA NJIA YA PICHA

    Bila shaka umeshakutana na aina nyingi za dawa za jamii ya antbiotic..Katika picha ni baadhi ya dawa hizo maarufu na matumizi yake kwa ufupi!Asnte na ni matumaini yetu utafaidika na makala hii fupi ya picha!

    Buswelu pharmacy,Mwanza

    VIDONDA VYA TUMBO (ULCERATIVE COLITIS)

    Ulcerative colitis
    Ulcerative colitis is an inflammatory bowel disease. Inflammation in the lining of the large intestine (the colon) causes ulcers to form. This can cause bleeding, diarrhea, weight loss, and fatigue.

    Ulcerative colitis is an autoimmune disease. That means the immune system, which normally helps fight off infections, mistakenly attacks the lining of the colon and rectum.

    Ulcerative colitis almost always involves the rectum. When confined to the rectum, the condition is called ulcerative proctitis. In most people, the inflammation spreads to involve more of the colon, often the entire colon.

    Ulcerative colitis can also cause inflammation in other parts of the body. These include the eyes, skin, liver, back, and joints.

    The cause of ulcerative colitis is still something of a mystery. The following factors likely play roles:

    - genes. Ulcerative colitis tends to run in families. Up to one in four people with ulcerative colitis has a parent or sibling with ulcerative colitis or with a related inflammatory bowel disease called Crohn's disease.
    - an overactive immune system. The immune system protects the body from infection by identifying and destroying harmful germs. In ulcerative colitis, the immune system does this but also attacks the lining of the large intestine.

    colitis

    Some people with ulcerative colitis have only occasional symptoms. For others, the symptoms are constant. The symptoms a person experiences can vary depending on the severity of the inflammation and where it occurs in the large intestine.

    Common symptoms include:

    - diarrhea, often with blood and mucus
    - cramping abdominal pain, especially in the lower abdomen
    - a frequent sensation of needing to have a bowel movement
    - little advance warning before a bowel movement
    - the need to wake from sleep to have bowel movements
    - feeling tired
    - loss of appetite
    - weight loss
    - fever
    - dehydration
    - low red blood cell count (anemia)

    Some people with ulcerative colitis develop pain or soreness in the joints, irritated eyes, and rashes.

    The symptoms of ulcerative colitis can suddenly get worse. This is called a flare. Then symptoms may fade away. This is called remission. Some individuals with ulcerative colitis have symptoms only rarely, others have flares and remissions, others have symptoms all or most of the time.

    Diagnosing ulcerative colitis

    There is no single, definitive diagnostic test for ulcerative colitis. If you have this condition, your symptoms and the results of various tests will fit a pattern over time.

    Some tests are often, but not always, abnormal in people with Crohn's disease:

    - blood tests can show a lot of white blood cells or other signs of inflammation, or anemia, a reduced number of red blood cells.
    - stool tests, also called feces or bowel movement tests, can detect white blood cells in the stool, a sign of possible ulcerative colitis, and also tell if an infection is causing the symptoms.
    - flexible sigmoidoscopy or colonoscopy lets a doctor look at the insides of the large intestine. This can reveal the presence of ulcers in the large intestine.
    - an x-ray or CT scan may be done to check for serious complications of ulcerative colitis, such as a perforated colon, or to determine how much of the colon is inflamed.

    Treating ulcerative colitis

    So far, there is no cure for ulcerative colitis. But there are ways to manage this condition to prevent flare-ups or reduce their intensity.

    Lifestyle changes

    Certain foods can trigger ulcerative colitis symptoms. Different foods affect different people. Common trigger foods include:

    - alcohol
    - milk, yogurt, cheese, and other dairy products
    - coffee, tea, soda, and other beverages that contain caffeine
    - fruit and juice
    - fried, fatty, and spicy foods
    - whole-grain and multigrain breads
    - condiments, such as ketchup, mustard, and mayonnaise
    - salad dressing
    - some vegetables, including cabbage, broccoli, and cauliflower
    - red meat
    - beans and lentils
    - spices and seasonings
    - artificial colors, flavors, and sweeteners

    To find out if any foods cause your symptoms to flare up, keep a food diary. Record exactly what you eat over several weeks, along with how you feel afterwards. When you look back, you may notice a pattern. If certain foods worsen your symptoms, talk to your doctor about eliminating them from your diet.

    Some people with ulcerative colitis don't get enough vitamins, minerals, and other important micronutrients, either because they eat less to avoid diarrhea or because the disease makes it difficult to absorb nutrients from food. Eating a well-balanced, nutritious diet can help. It may also be necessary to take a multivitamin, multimineral supplement.

    Non-steroidal anti-inflammatory drugs such as aspirin, ibuprofen, and naproxen can trigger or worsen the symptoms of ulcerative colitis. A better choice for pain relief is acetaminophen.

    Medication

    Medications cannot cure ulcerative colitis, but they can stop or ease symptoms. They work by quelling inflammation in the intestine:

    - aminosalicylates. These anti-inflammatory drugs, which are related to aspirin, are used to ease mild to moderate symptoms or to help people stay symptom-free.
    - corticosteroids. These drugs quiet the immune system and decrease inflammation. They can also help stop or ease symptoms. Corticosteroids are usually used when symptoms do not respond to aminosalicylates. Because of potential side effects, they are not usually used long-term.
    - immunomodulators. These medications reduce the activity of the immune system. This reduces inflammation in the colon, which can help keep a person symptom free. Immunomodulators can take up to three months to start working. They are usually needed when aminosalicylates alone do not keep inflammation controlled.
    - biologics. These drugs target a protein made by the immune system. They decrease inflammation in the large intestine and can also quickly stop symptoms.

    Other medications that may be needed include:

    - acetaminophen, to relieve pain
    - antibiotics, to prevent or treat bacterial infections in the gastrointestinal tract
    - medication to slow or stop diarrhea
    - medication to decrease spasms of the colon

    Surgery

    Surgery to remove the colon and rectum may be an option for people who have:

    - severe symptoms not controlled by medicine
    - unacceptable side effects from medicine
    - a very high risk of colon cancer because of long-lasting inflammation throughout the colon

    Surgery involves removing the colon and some or all of the rectum and anus. There are two types of surgery for ulcerative colitis:

    The surgeon removes the entire colon and rectum and then creates an opening in the abdominal wall. The end of the small intestine is attached to this opening. After this procedure, waste leaves the body through the opening in the abdominal wall, rather than through the anus. A bag attached to the opening collects the waste.

    The surgeon removes the colon and then connects the small intestine to the anus. After this procedure, normal bowel movements still occur.

    Ulcerative colitis and colorectal cancer

    Ulcerative colitis increases the risk of colorectal cancer. Colorectal cancer often begins as small growths (polyps) on the inside of the large intestine. The risk of colorectal cancer increases based on:

    - the length of time a person has had ulcerative colitis
    - how much of the colon is affected by ulcerative colitis

    People with ulcerative colitis should have more frequent tests for polyps and colorectal cancer than people at average risk. The gold standard screening test is a colonoscopy. Polyps can be removed during a colonoscopy. This reduces the risk of colorectal cancer. Ask your doctor how often you should be checked for colorectal cancer.

    Surgery to remove the entire colon eliminates the risk of colon cancer.

    Wednesday, 13 July 2016

    KUKOSA HEDHI KWA WANAWAKE (AMENORRHEA)

    Absent Periods

    In many cases, absent periods aren't a cause for concern. However, sometimes an underlying medical condition can be responsible that will need to be investigated and treated.

    Some girls won't start their periods by the expected age, and there are various reasons why periods might naturally stop at certain times.

    For example, your periods will stop during pregnancy, while you're breastfeeding, or after the menopause. Some types of contraception can also cause you to temporarily stop having periods.

    Underlying medical conditions

    The medical name for absent periods is amenorrhoea. The lack of periods can sometimes be a sign of an underlying medical condition, such as:

    - polycystic ovary syndrome (PCOS) – a condition where the ovaries don't regularly release an egg (ovulate)
    - hypothalamic amenorrhoea – where the part of the brain that regulates the menstrual cycle stops working properly; this is thought to be triggered by excessive exercise, excessive weight loss, or stress
    - hyperprolactinaemia – where a person has abnormally high levels of a hormone called prolactin in their blood
    - premature ovarian failure – where the ovaries stop working properly in women who haven't yet reached the age of natural menopause (usually from the age of 50)

    When to seek medical advice

    You should see your GP if you're worried about any problems with your periods so they can try to find the cause.

    Depending on what your GP thinks may be causing your absent periods, you may be referred to a specialist for further investigation and any necessary treatment.

    Who's affected?

    It's relatively common to stop having periods after previously having them. This is known as secondary amenorrhoea, and it's estimated to affect around 1 in 25 women at some point in their lives.

    It's more common in teenage girls and younger women, particularly in certain groups, such as professional athletes, dancers and gymnasts.
    Not starting your periods by the expected age (primary amenorrhoea) is much less common. It's estimated to affect 1 in every 300 girls.

    Treating absent periods

    The treatment for absent periods will depend on the cause. For example, PCOS can often be controlled using hormonal treatments, while women with hypothalamic amenorrhoea will often start to have regular periods if they cut down on exercise and reach a healthy weight.

    In some cases, your doctors may recommend waiting to see if your periods return or start on their own.

    Sometimes it isn't possible for periods to be restored with treatment. This is usually the case with absent periods caused by premature ovarian failure.

    The menstrual cycle

    Periods are part of the menstrual cycle, which usually starts when a girl is around 12 years old, but it can be earlier or later than this.

    Roughly every 28 days, a woman's ovaries will release eggs – as long as she hasn't had the menopause. This is known as ovulation.

    The lining of the womb will thicken to prepare for the eggs. If the eggs aren't fertilised by sperm, the thickened lining will break down, resulting in bleeding from the vagina (a period).

    Tuesday, 5 July 2016

    HERNIA-NGIRI

    Maelezo ya hernia kwa njia ya picha..Wengi wana tatizo lakini hawana taarifa ya kutosha juu ya tatizo hilo!karibu upate maelezo ya picha na jinsi ya kudeal na tatizo!

    Scroll to Top