728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday 12 May 2016

    FAHAMU BAWASIRI AU HEMORRHOID NA JINSI YA KUIEPUKA

    FAHAMU UGONJWA WA BAWASIRI AU KUOTA KINYAMA SEHEMU YA HAJA KUBWA (HEMORRHOID) NA NAMNA YA KUEPUKA NA UGONJWA HUU
    ~watu wengi wanasumbuliwa na tatizo hili ambalo huwafanya kuwa na uoga na aibu wa kuelezea na kushindwa hata kwenda hospital kupata tiba
    JE, UNAJUA BAWASIRI/HEMORRHOIDS NI NINI????!!
    ~Ni ugonjwa unaotokana na kuathirika kwa mishipa ya damu ya ndani na nnje ya sehemu ya haja kubwa na wakati mwingine mishipa hiyo huweza kupasuka/kuteleza na kuvuja damu kwenye njia ya haja kubwa na kasababisha kutoka kinyama au uvimbe
    ~ugonjwa huu wa bawasiri kwa lugha ya kitaalamu tunauita HEMORRHOIDS ilhali kwa lugha ya kingereza unafahamika kama piles
    ~tatizo hili huwaathiri watu wote ila zaidi huwaathiri watu wazima kuliko watoto na inakadiriwa kuwa karibu 50%ya watu wote wako katika hatari ya kupata tatizo hili katika umri wa miaka 30_50
    AINA ZA BAWASIRI
    ~Kuna Aina mbili za bawasiri
    (A) BAWASIRI YA NDANI
    ~Aina hii ya bawasiri hutokea ndani ya mfereji wa haja kubwa huwa haiambatani na maumivu na wengi huwa hawajitambui kuwa Wana tatizo hili
    ~Aina hii hutokana na kuvimba na kuharibika kwa mshipa wa artery za ndani ya mfereji wa haja kubwa
    ~Aina hii imegawanyika katika madaraja manne
    (1)DARAJA LA KWANZA ~Hii ni bawasiri ambayo haitoki mahal pale panapohusika
    (2)DARAJA LA PILI ~hii  hutokea wakati wa haja na kurudi yenyew ndani baada ya kujisaidia
    (3)DARAJA LA TATU :hii hutokea wakati wa haja kubwa na mtu kuweza kurudisha ndani yeye mwenywe
    (4)DARAJA LA NNE :hii ni bawasiri inayotoka na huwa ngumu kurudi
    (B)BAWASIRI YA NNJE
    ~Aina hii ya bawasiri hutokea katika eneo la mwisho kabisa la mfereji wa haja kubwa na huambatana na maumivu makali na kuwashwa kwa ngozi katika eneo la tundu Hilo pia husababisha mishipa ya damu (vena) kupasuka na damu kuganda na kasababisha Aina ya bawasiri iitwayo THROMBOSED HEMORRHOIDS
    CHANZO CHA TATIZO
    ~chanzo halisi cha ugonjwa huu hakijapatikana ila Kuna vitu ambavyo huwa chanzo cha kupata ugonjwa wa bawasiri ambayo ni ÷
    👉KUFANYA MAPENZI KINYUME NA MAUMBILE
    👉KUHARISHA KWA MUDA MREFU
    👉TATIZO LA KUTOPATA CHOO
    👉MATATIZO YA UMRI
    👉KUKAA KITAKO KWA MUDA MREFU
    👉UZITO KUPITA KIASI
    👉MATUMIZI YA VYOO VYA KUKAA KWA MUDA MREFU

    DALILI ZA BAWASIRI
    👉Ngozi kuwasha katika eneo la tundu la haja kubwa
    👉kupata maumivu makali wakati wa kujisaidia
    👉kutokea uvimbe katika eneo la tundu la haja kubwa
    👉kujitokeza kwa kinyama katika eneo la tundu Hilo
    👉kinyesi kuwa na damu na kunuka harufu mbaya sana

    MATIBABU NA JINSI YA KUEPUKA TATIZO LA BAWASIRI
    ~matibabu ya bawasiri hutegemea na Aina ya bawasiri pia tiba iliyozoeleka ni kukatwa kinyama na kuendelea na lishe ya chakula hata hvyo tiba hii si nzuri kwasababu huwa haitibu chanzo cha tatizo hivyo huwa rahisi kujirudia hivyo tiba nzuri ni kutumia dawa aina ya  TCM CAPSULE  kwani ni nzuri huwa zinatibu chanzo na kumaliza tatizo kabisa
    ~Pamoja na hayo bawasiri ni ugonjwa unaoweza kuepukika kwa kuzingatia yafuatayo
    👉KULA MBOGAMBOGA ZA MAJANI, MATUNDA, NA NAFAKA ZISIZOKOBOLEWA
    👉KUNYWA MAJI MENGI ANGALAU GRASS 6/12 Kwa siku
    👉EPUKA KUKAA  CHOONI KWA MUDA MREFU
    👉FANYA MAZOEZI MEPESI
    👉EPUKA KUFANYA MAPENZI KINYUME NA MAUMBILE

    MADHARA YA TATIZO LA BAWASIRI ugonjwa wa Bawasiri usipotibiwa huleta athari zifuatazo Kwa Mgonjwa
    👉kupata upungufu wa damu (anemia)
    👉Kupata tatizo la kutokuweza kuhimili choo
    👉hupunguza nguvu za kiume na kuondoa hamu ya tendo la ndoa kwa wanawake kwasababu husababisha maumivu Kwa Mwanamke wakati wa tendo la ndoa
    👉kuathirika kisaikolojia
    👉kukosa moral ya kufanya Kaz kutokana na maumivu makali
    NOTED :NDUGU RAFIKI KAMA UNA UGONJWA HUU EPUKA KULA NYAMA NYEKUNDU NA PILIPILI PIA UNAWEZA  WASILIANA NAMI KWA USHAURI WA MATIBABU YA KUONDOA TATIZO HILI PASIPO KUFANYA UPASUAJI
    Asante kwa kuwa nami kupata elimu hii rafiki kama una maswali/maoni au mapendekezo yoyote niandikie kupitia namba na email yangu hapo chini

    Makala hii imeandaliwa na Dr Naytham nsalum998@gmail.com/0689538628
    PLZ USISAHAU KUSHARE, KULIKE NA WATAG RAFIKI ZAKO

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: FAHAMU BAWASIRI AU HEMORRHOID NA JINSI YA KUIEPUKA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top