728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday 3 August 2016

    MBA AU PITYRIASIS VERSICOLOR

    Huu ni ugonjwa wa ngozi ambao hupata mtu hasa maeneo ya shingoni,kifuani na mgongoni na muonekano wake ni kama mabaka madogo madogo meupe.
    Ni ugonjwa wa fangasi wajulikanao kama pityriasis versicolor na mara nyingi haujionyeshi mpaka hali ya joto,unyevu au wakati wa ujauzito.
    Pia hizi mba huweza kuanzia kichwani yaani dandruff baadae hushuka mpaka maeneo ya shingoni na mgongoni..Usipotumia tiba vyema ugonjwa huu ni rahisi sana kujirudia rudia.
    KINGA NA TIBA
    -fanya scrub ili kuondoa wadudu au maeneo yalnayoanza kuathirika
    -usitumie vaseline,olive oil au mafuta ya nazi kwani huongeza joto na kuvipa nafasi ya kukua kirahisi
    -Tumia imidazole cream kama clotrimazole cremas maeneo yaliyoathirika kwa week 4.
    -Unaweza kuongezea selenium sulfide shampoo au ketaconazole 2% shampoo japo gharama kidogo.
    Unaweza kutumia sulfur+salicylic acid ointment kila siku usiku kwa week 2 hadi 4
    -unaweza pia kutumia sulfur ointment kama kinga kwa kupaka usiku kwa week 2
    -Kama ugonjwa ni wa muda mrefu na unaojirudia rudia basi tumia vidonge vya ketaconazole au itraconazole..ketaconazole 400 mg kama start dose au 200 mg kila siku mara moja kwa siku 5.
    Tiba hukamilika pa le tu madoa au mba yanapokuwa yamekwisha kabisa na kama madoa bado yapo basi ujue bado fangasi hao wako active.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MBA AU PITYRIASIS VERSICOLOR Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top