Chunusi ni nini?
Chunusi ni sababu iliyozoeleka ya kutokea kwa
mabaka kwa watu kuanzia umri wa miaka 12 na 25 na wakati mwingine kwa watu
wenye umri zaidi ya hapo. Wavulana huathriwa zaidi kuliko wasichana na mara
nying huathiri maeneo ya uso, mgongo, shingo na kifuani.
Hali hii isipotibiwa inaweza kukaa kwa zaidi
ya hata miaka 5 kabla ya kuondoka kabisa lakini pia kwa baadhi ya watu huweza
kukaa zaidi.
Nini Husabababisha Chunusi?
Ijue Ngozi Kwanza kwa ufupi
Kuielewa ngozi: Chini ya ngozi kuna tezi (Sebaceous gland)
ambayo hufanya kazi ya kutengeneza mafuta mafuta ya ngozi (Sebum) . Pia kwenye
ngozi kuna matundu madogo (pores) ambayo hurusu mafuta kutoka kwenye tezi kuja
nje ya ngozi, pia kuna vinyweleo ambavyo vinaota kwenye matundu haya.
Ukiwa kijana
unatengeneza mafuta zaidi ya ngozi kuliko ukiwa mdogo na hii huchangiwa na
ukuuaji na mabadiliko ya homoni mwilini au puberty ambayo huchochea kuzalishwa
kwa mafuta
Ni lazima kuwa kama
mwili utatengeneza mafuta zaidi ngozi itakuwa ya mafuta zaidi yaani greasy na
ndivyo hatari ya kupata chunusi inakuwepo. Baadhi ya watu hutengeneza mafuta
haya mengi zaidi kuliko wengine.
Hatua za Chunusi: Baadhi ya vitundu huzibwa na mafuta yanapozidi
mwilini na hii ni kwa sababu ngozi ya juu vitundu vinajaa mafuta na baadhi ya
chembe hai za ngozi (skin dead cells) ambazo zinajazana kwenye vitundu kwa juu.
Unaweza kuona sehemu ya uchafu (Pulgs) unaoziba vitundu kwa juu kama baka dogo lijulikanalo
kama black heads na whiteheads (comedones)
Angalizo:
Baka au weusi unatokana na rangi ya ngozi au skin pigment na mara nyingi si
chafu kama inavyofikiriwa. Mara nyingi chunusi haiwezi kukua zaidi ikishafikia
hali hii ya comedones.
Mara nyingine mafuta
hujilundika chini ya vitundu vilivyozibwa, hali hii inapotokea huitwa pimples
au papules na hii ni hatua isiyo hatari sana kwenye chunusi.
Chunusi zilizokithiri: mafuta yanapozibwa husababisha baadhi ya
bacteria kama Propioni bacterium acnes kukaa na kuzaliana kwenye vitundu vya
ngozi na mara nyingi bacteria hawa huwepo kwenye ngozi bila madhara makubwa
kwenye ngozi ila wakizidi huleta Sasa
wanapozidi hufanya mwili kupigana na hao bakeria na kusababisha uvimbe kwenye
ngozi (Inflammation) na ngozi kuonekana nyekundu na vinundu kukua na kuwa na
usaha (Pustules) na mara nyiningine hukua zaidi na kuonekana kama jipu (Nodules
au cysts)
Mara
nyingi chunusi hizi hupona zenyewe na wakati mwingine huacha baka baada ya
inflammation kuondoka nah ii huonekana zaidi kwa watu weusi Huacha vikovu
vidogo huondoka taratibu na kuweza kuacha alama kwenye ngozi.
BAADHI YA SABABU ZA CHUNUSI
Maelezo ya juu ni
namna chunusi inavyoweza kutokea, lakini pia baadhi ya magonjwa huweza
kusababisha kutokea kwa chunusi kwa wanawake kwa mfano uvimbe kwenye yai au
mirija ya uzazi pamoja na uzalishaji wa homoni za kiume kwenye yai la kike au
tezi la adrenali.Hali hizi au magonjwa haya husababisha vinyweleo kusinyaa
mbali na chunusi pia husababisha wingi wa vinyweleo (hairsutism). Vilevile
kemikali pia husababisha kutokea kwa chunusi (Halogenated hydrocarbons)
Kitu
gani kinaongeza chunusi na kuleta madhara kwenye ngozi?
·
Vidonge
vya majira.
·
Mabadiliko ya homoni
kwa wanawake hasa wakati wa hedhi huleta vichunusi
·
Vipodozi na make ups
huongeza chunusi lakini make up mara nyingi hazizidishi chunusi na inashauriwa
kutumia vipodozi ambavyo havina mafutaau oil
·
Kutumbua chunusi
kunaongeza uvimbe na madoa.
·
Kutoka
jasho sana au hali ya hewa ya joto na unyevu, jasho jingi huziba vitundu vya
hewa vya ngozi
·
Nguo kubana hasa
vilemba na sidiria kutokana na jasho na msuguano
·
Utumiaji wa baadhi ya
dawa kama phenytoin kwa ajili ya kifafa au cream na ointment za steroids.
·
Baadhi husema vyakula
vyenye sukari na maziwa huongeza chunusi lakini hakuna uthibitisho wa kitaalamu
kwenye hili.
Some myths about acne-Ukweli
dhidi ya uzushi kuhusu chunusi
·
Chunusi inasababishwa
na kutooga,
·
Mawazo au stress yanaleta chunusi
·
Chunusi sio infection
pekee bali ni mchanganyiko wa kubadilika kwa homoni za mwili, mafuta ya ngozi
au sebum na bacteria wa ngozi kuwa wengi kuliko kawaida.. Chunusi haiambukizwi
kwa kugusana
·
Huwezi kutibu chunusi
kwa kunywa maji mengi.
·
Huwezi kutibu chunusi
kwa kuota jua.
·
Wengine huamini kuwa
chunusi haitibiwa na dawa, sio kweli kama ukitumia dawa vizuri unapona chunusi
kabisa.
Jinsi
ya kutunza ngozi kwa mtu mwenye chunusi
·
Usioshe uso mara kwa
mara, kwa kawaida mara mbili kwa siku inatosha sana. Tumia maji ya uvugu vugu
kwani maji ya baridi au moto yatafanya hali ya chunusi kuwa mbaya zaidi.
Usisugue uso sana na badala yake tumia kitambaa laini na
·
Kutumia sabuni zenye
dawa (Antiseptic washes) husaidia.
·
Huwezi kuliondoa baka
la chunusi kwa kusugua kwani ni sehemu ya ngozi yenye rangi yaani skin pigment (melanin)
·
Baadhi ya cream
husaidia hasa ambazo hazina manukato na zile zinazoleta unyevu kwenye ngozi (fragrance-free,
water-based moisturising cream). Usitumie cream zenye mafuta mengi kwani
zinaziba vitundu vya hewa vya ngozi.
Malengo ya kutibu
chunusi: Malengo ni kuondoa
mabaka na makovu kadri inavyowezekana. Tiba inaweza kuwa ya kupakaa au vidonge..
Unaweza pia usitumie
chochote kwa chunusi ambayo haijavimba na kuwa kubwa. Chunusi ndogo ndogo
hazina madhara sana na hupata watu wengi bila kuwaharibu, ila chunusi zilizovimba
na kweka kitu kama usaha sio nzuri na unaharibu uso na tiba ni muhimu kuzuia
mabaka na makovu
Dawa za kupakaa: baadhi ya gels, cream na lotion hutumika kutibu chunusi na
hufanya kazi tofauti tofauti. Ni vyema kusoma kipeperushi cha dawa kabla
hujaanza kuitumia na ni muhimu kuitumia eneo lililoathirika au kuzunguka eneo
hilo pekee
Benzoyl peroxide inaweza kupakwa kwenye ngozi na inaua bacteria, kupunguza
uvimbe wa chunusi na kupunguza kuziba kwa vitundu vya hewa vya yaani to unplug blocked pores. Hupatikana kwa
majina tofauti tofautiTherefore, it often works well to clear inflamed spots
and it helps to clear bna nguvu kama: 2.5%, 4%, 5% na 10%
Benzoyl peroxide:
·
Hubadili rangi ya
nywele pamoja na baadhi ya vitambaa unavyotumia kupakaa.
·
Husababisha ngozi
kuwasha na kama hali hiyo ikitokea unashauriwa kuacha kwa muda na kutumia yenye
nguvu kidogo au punguza muda wa kutumia kwa siku badala ya mara mbili unaweza
kupakaa mara moja kwa siku. Ili kupunguza kuwasha unatakiwa kufanya yafuatayo:
·
Wengi inawakubali
yenye nguvu ya 5% kama ikileta madhara jaribu 2.5% na ukipenda yenye nguvu
zaidi basi tumia kidogo kidogo.
·
Tumia iliyochanganywa
na maji na sio alcohol-based.
·
Pakaa kwa mara moja
kila siku unapoanza kuitumia na baada ya masaa unaitoa na endelea kuongeza
kidogo kidogo muda wa kuiacha kwenye ngozi.
·
Ikishakuzoea tumia
mara mbili kwa siku.
Retinoids ni nzuri
kwenye kuondoa vitundu vilivyoziba. Ina majina mengi na inahusisha adapalene, tretinoin na isotretinoin ambazo huja kwa majina tofauti tofauti
ya kibiashara. Husaidia pia kupunguza uvimbe wa chunusi. Unahitaji cheti
kutumia dawa hizi. Unapotumia dawa
hizi;
·
Unaweza kupata wekundu
kwenye ngozi na wakati mwingine ngozi kubanduka lakini hali hurudi kawaida
jinsi unavyoendelea kuitumia.
·
Mwanzoni inaweza
kuzidisha chunusi lakini zitpungua unapoendelea
·
Unapozitumia hizi,
usikae kwenye mwanga wa jua na vizuri ukazitumia usiku na kuosha
·
Madhara makubwa
unapotumia hizi dawa au kemikali ni kuwashwa, kuungua au ngozi kuwa kavu. Hivyo
unapoanza kutumia inakulazimu kutumia ambayo haina
·
Haitakiwi kuwa
mjamzito unapozitumia kwani huweza kuathiri kiumbe cha tumboni.
Antbiotics au Kemikali za kuua
Bakteria: Zinapopakawa kwenye
ngozi huua bacteria na kupunguza uvimbe wa chunusi. Lakini hazisaidii sana
kwenye kuzibua matundu ya ngozi hivyo ni nzuri kwenye kutibu chunusi lakini
hazisaidii kuondoa madoa doa. Hivyo hizi dawa hutolewa pamoja na cream au dawa
zingine ili kutibu kabisa chunusi. Pia ni muhimu kuzitumia kwa tahadhari kwani
bacteria zina tabia ya kuzoea hizi dawa na kwa baadae kushindwa kuziondoa
(resistance)
Azelaic acid huzibua vitundu vya hewa na haisababishi
kuwashwa kwa ngozi kama retinoids na zinapunguza uvimbe pia lakini si kwa kiasi
kikubwa kama.
Mchanganyiko wa dawa
husaidia sana kutibu kabisa chunusi na baadhi ya vipodozi unakuta zina benzoyl
peroxide na antibiotic,au retinoid na
antibiotic. Mchanganyiko hufanya kazi zaidi kuliko dawa ikiwa pekee.
Vidonge
vya Antibiotics: Husaidia kuua bacteria, kupunguza uvimbe
Hazisaidii sana kwenye
kuzibua vitundu vya ngozi hivyo ni vyema kutumia na cream zenye benzoyl
Tetracycline-based
antibiotics ni nzuri kwa kutibu chunusi kuliko zingine na hizi ni kama
vile; oxytetracycline, tetracycline, doxycycline na lymecycline.
·
Watoto chini ya miaka 12
hawtakiwi kutumia hizi antibiotics za tetracycline.
·
Kwa wajawazito,
wanaonyonyesha au unategemea ujauzito hushauriwi
·
Chakula na maziwa
zinazuia kufanya kazi kwa oxytetracycline au tetracycline. Hivyo ni vyema
kuzinywa kabla ya kula na tumia maji badala ya maziwa. Doxycycline na
lymecycline hizi unaweza kuzinywa hata ukiwa umekula teyari.
Tiba kwa njia ya homoni
Vidonge vya majira (The combined contraceptive pill) zinaweza kusaidia iwapo chunusi zako
zimetokana na mabadiliko ya homoni kwa mfano chunusi zinazojitokeza ukubwani au
wakati wa hedhi.
Ni homoni ya oestrogen
ambayo ipo kwenye kidonge cha majira ndio inayosaidia. Kidonge chenye co-cyprindiol, husaidia pale inapobainika homoni ya androgen imesababisha chunusi.Kwa
mfano kukua kwa nywele usoni pamoja na chunusi co –cyprindol inafaa kwani ina
mchanganyiko wa oestrogen na cyproterone (ant androgen)
Isotretinoin hupunguza
kuzalishwa kwa mafuta ya ngozi (sebum) ambayo inatengenezwa na sebaceous
glands. Hufanya kazi vizuri kwa kuondoa mabaka hata yale sugu. Hata hivyo
hutumiwa baada ya ushauri wa mtaalamu.
Ni muda gani unahitaji
kutibu chunusi ?
Ili uanze kuona
maendeleo mazuri kwa tiba yoyote utalazimika kutumia kwa mwezi mzima na
maendeleo mazuri huonekana baada ya wiki ya sita au zaidi. Chunusi nyingi
haziishi kwa sababu watu wengi hufikiria chunusi hutibiwa kwa siku kadhaa hivyo
huacha tiba
Hivyo ni vyema kutumia
dawa au kipodozi kwa wiki sita kabla ya kumua kuacha au kusema hakija kusaidia.
Ni vyema kubadili dawa kama hakuna matokeo mazuri au kuongeza dawa au kipodozi
kwenye kile ulichoanza na usiache kabisa.
Je, Chunusi inaweza kurudi baada ya Tiba?
Ukiacha tiba chunusi
hurudi ni vyema kuendelea na tiba mpaka ziishe kabisa. Kwa watu wengine hutumia
mpaka miaka 5 kuweza kupona kabisa au kufikia umri mkubwa wa kuacha kuzalisha
sebum. Tumia benzoyl peroxide au topical
retinoid kama muendelezo wa tiba ya chunusi.
Antibiotics hutumiwa
mara moja na baada ya hapo endeleza kupakaaa kwenye ngozi dawa zilizotajwa hapo
juu
Je unahitaji kwenda hospitali kwa ajili ya chunusi?
Chunusi isipopona
unashauriwa kwenda hospital na kumuona daktari, pia baadhi ya makovu huweza
kuondolewa na dakatri mtaalamu na ngozi yako kuonekana vizuri.
Nashukuru kwa kupitia makala hii naumefaidika na kitu..Siku njema!
Prepared by: Buswelu pharmacy +255767650213
Ilemela, Mwanza
0 comments:
Post a Comment