728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, 31 July 2016

    FANGASI KATIKA VIDOLE VYA MIGUU|ATHELETES FOOT

    Athlete's foot ni aina ya ugonjwa wa ngozi unaotokea katikati ya vidole vya miguu (in between toes)..Huwasha,na mara nyingi hufunikwa na gamba nyeupe kati ya vidole vya miguu..Na mara nyingi huwa kati ya kidole cha nne na cha tano cha mguu!
    Hii hali sio mara zote ni fangasi pekee hata bakteria huweza kuleta hali hiyo au mchanganyiko wa wadudu hao wote kwa pamoja.

    Hali hii hujitokeza sana kwa watu wanaovaa viatu vya raba au boots na plastic sandshoes..Hali hii isipotibiwa mapema huleta harufu na tiba yake kuwa ngumu au complicated.

    KINGA NA TIBA

    -Weka ukavu katikakati ya vidole vyako vya miguu..Hii unaweza kulifanya pale unapooga au kunawa hakikisha unajikausha vyema sehemu hizo (keep the space in between the toes dry)
    -Tumia betadine scrub au GV
    -Tumia soksi za pamba na usivae viatu vinavyobana na kuleta joto miguuni
    -Kubadili soksi kila siku kunasaidia kuzuia kupata maambukizi tena

    -Tumia Imidazole cream au whitefield ointment kila siku mara mbili kwa muda wa wiki au zaidi na mara nyingi mpaka wiki 4.

    Karibu buswelu pharmacy, Ilemela Mwanza kwa ushauri na tiba +255767650213.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: FANGASI KATIKA VIDOLE VYA MIGUU|ATHELETES FOOT Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top