728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday 26 July 2016

    Je,Ni salama kutumia dawa iliyokwisha muda wake?

    Nini maana ya expired medicines?

    Ni siku ya mwisho ambapo mtengenezaji wa dawa (Manufacturer)  amekuhakikishia (Gurantee) usalama na ufanyaji kazi bora wa dawa husika (Safety and Potency).

    Mara nyingi huwekwa kwenye makasha (Containers) ya dawa kama alama (Labels) na hata vyeti vya dawa (Prescriptions). Pia tarehe ya kikomo ya dawa (Expiration date) huwa inapimwa kupitia jaribio la  uimara (Stability testing) chini ya njia bora za uzalishaji (Good manufacturing practices) zilizowekwa na mamlaka zinazosimamia watengeza dawa kwa nchi husika mfano TFDA kwa Tanzania.

    Kwa ufupi ni kuwa dawa inapotengezwa, muda ambao dawa itakuwa na nguvu na kuanza kupoteza nguvu hupimwa (Shelf life). Mtengeneza dawa hufanya hivyo kukuhakishia kuwa dawa inapotumika ndani ya huo muda wa kuwa na nguvu itafanya kazi kwa kiwango cha juu cha ubora na usalama wake (Potency and safety)

    Je, Dawa huisha nguvu na usalama mara tu pale tarehe ya kikomo ilivyowekwa?

    Tafiti nyingi zimeonyesha kuwa bado dawa nyingi zina ubora na usalama hata baada ya kupita tarehe ya kikomo cha dawa kama ilivyoandikwa kwenye kasha hasa dawa zenye umbile la vidonge na capsules kwani ni imara (Stable). Lakini mara nyingi ni ngumu kuweza kujua kuwa ni siku gani hasa ubora au usalama huo wa dawa umekwisha kabisaa.

    Madhara

    Kutumia Dawa iliyokwisha nguvu na usalama (Sub potent medicines) ni hatari kwa afya. Kwani inaweza kuleta madhara kama usugu wa vijidudu vya magonjwa hasa bakteria na hata kifo. Dawa zinazotolewa kwa njia ya sindano pia si salama kuzitumia baada ya kuisha  muda kwani zinaweza kusababisha madhara makubwa kwani vijidudu (kama fungasi na bakteria) huweza kuota kwenye dawa hizo zenye asili ya majimaji au powder na kuleta madhara makubwa zaidi endapo wataingia mwilini

    Dawa za kutibu kisukari kwa mfano huwa ni rahisi kupungua kiwango cha kutibu (Susceptible to degration) mara tu baada ya siku au tarehe ya kikomo.

    Hata hivyo wataalamu wanashauri utunzaji ulio bora wa dawa (Storage) unaweza kusaidia kuendelea kwa nguvu ya dawa (Therapeutic effect) hata baada ya tarehe ya mwisho ya kutumia. Dawa mara nyingi hubaki na uimara wake inapotunzwa kwenye ukavu, sehemu yenye ubaridi baridi na mbali na joto au mwanga wa jua.

    Baadhi ya dawa nyingine kama antibiotiki inayoitwa Tetracycline hugeuka kuwa sumu baada ya muda wake wa matumizi kuisha na huweza kusababisha matatizo kwenye figo

    Je, Ni sawa kwa mgonjwa kutumia dawa iliyofikia tarehe ya kikomo ?

    Ni vyema kubadili dawa pindi tu unapogundua imefikia tarehe ya kikomo. Japokuwa hakuna uthibitisho wa moja kwa moja wa kwamba si salama kunywa dawa iliyofika kikomo, lakini kwa magonjwa yanayohatarisha maisha (chronic and life threatening diseases) kama ya moyo, kifafa, allergy ni ushauri uliowazi kabisa si vyema kutumia dawa hizo baada ya tarehe ya kufika kikomo (Expired date). Kwa ufupi ni Kwamba ni nani ambaye yuko tayari kuhatarisha maisha au afya yake. Chukua tahadhari!!!

    Cha kujifunza

    Tarehe ya mwisho ya kikomo cha dawa imewekwa kama kipimo (Conservative measure) ili kukuhakishia uinatumia dawa iliyo na uimara wa kufanya kazi (Highest potency).

    Wakati unaumwa, unachofikiria kwa haraka ni kupona mara moja. Kutumia kitu ambacho una kiamini kama tiba ndio jambo la msingi kuliko kutumia kitu chenye kukuletea mashaka.

    Mbali ya kuwa dawa nyingi zimewekewa alama za muda wa kuisha, lakini utunzaji wa dawa mzuri bado ni njia bora Zaidi ya kuhakikisha uimara wa dawa hiyo (Effectiveness)

    Asante.

    By Mafamasia, Michael Bajile
    January 2015

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Je,Ni salama kutumia dawa iliyokwisha muda wake? Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top