728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday 25 July 2016

    ‘Hata nitakapotangulia mbele ya haki niiache Tanzania ikiwa na amani’ -Rais JPM


    July 25 2016 Serikali ya Tanzania imefanya  maadhimisho ya siku ya mashujaaambapo mgeni rasmi alikuwa ni Rais John Pombe Magufuli alikuwa mgeni rasmi katika maadhimisho hayo yaloiyofanyika kitaifa Dodoma.
    Katika hotuba yake Rais Magufuli hakuacha kusisitizia suala la amani katika taifa huku akiwataka watanzania wote kwa pamoja kuhakikisha wanailinda na kuidumisha.
    Tunapoadhimisha siku ya mashujaa, tunawakumbuka wote waliotoa uhai wao kuhakikisha nchi inakuwa na amani, hawa mashujaa wetu waliofariki hawakujali dini, vyama wala makabila yao, tunapowakumbuka tuilinde amani‘ –Rais Magufuli
    Niviombe vyama vyote wawe wahubiri wa amani kwakuwa  maendeleo ya nchi yetu yatapatikana kama tutailinda amani tuliyonayo, hata nitakapotangulia mbele ya haki niiache Tanzania ikiwa na amani’ –Rais Magufuli
    Lakini pia Rais Magufuli hakulikalia kimya hili la mpango wa Serikali kuhamishia makazi yake Dodoma ambapo amesema …>>>’Haiwezekani Serikali ninayoiyongoza ishindwe kuhamia Dodoma, leo tunamkumbuka pia baba wa taifa aliyesema makao makuu yawe Dodoma, sisi hatuwezi kupinga hatua hiyo‘ –Rais Magufuli
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: ‘Hata nitakapotangulia mbele ya haki niiache Tanzania ikiwa na amani’ -Rais JPM Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top